Watu wengi wanasubiri kuona tangazo la ujio wa simu mpya. Yaweza kuwa iPhone 13 ama wanavyoweza kuamua kuiita.
Lakini ikiwa ni nusu mwaka tangu kutoka kwa iPhone12, tetesi juu ya ujio wa toleo jipya la simu zinazidi kuzagaa na wataalam wa masuala ya teknolojia wameanza hata kutabiri nini kitakuwemo kwenye simu hizo.
Wengi wanaamini kwamba haitakuwa na tofauti kubwa kimuundo ukilinganisha na iPhone12 mini, lakini itakuwa na nyongeza za mambo mengine.
Mtandao maarufu na unaoheshimika kwenye masuala haya na ushauri wa ununuzi wa vitu vya kiteknolojia wa TechRadar wameandika hapa kwamba wanaamini wanajua baadhi ya mambo kuhusu ujio huo mpya. Hata bei na wakati inapoweza kuwasili.
Wasome